|
1.Zefania
2:3;3:12-13
|
2.1Kor 1:26-31
|
Injili:
Mt5:1-12
|
" Njia itupelekayo kwenye raha ya
milele"
Wapendwa taifa la Mungu
niwakaribishe katika tafakari ya masomo yetu ya jumapili ya nne ya kipindi cha
kawaida cha mwaka wa Kanisa mwaka A. Neno linalotuongoza leo katika tafakari
yetu ni, ' ni njia ipi hasa inatupatia raha ya milele katika maisha yetu?"
Kitu ambacho hutuangaisha sisi binadamu hapa duniani daima huwa ni kutafuta
chochote ambacho hutufanya tuwe na raha na hatimaye kufurahi' au tuseme daima
binadamu huangaika hapa na pale ili mwisho wa siku apate raha au aweze
kustarehe, hilo ni jambo ambalo kila mmoja wetu hulitafuta kwa gharama yoyote
ile. "Hata hivyo tatizo ni kwamba
kile watu wakifikiricho kuwa kitawaletea raha daima katika maisha, kimsingi
huwa hicho hakileti raha ya kweli" ( Aristotle).
Hebu chukulia mfano wa
yule mtu anayeamini kuwa akinunua chupa ya bia, au chupa ya whisky akainywa
kwake anafikiria kuwa hiyo inamletea raha. Huyo mtu akinywa chupa ya bia au whisky na akaendesha
gari lake kurudi nyumbani kwa sababu ya ulevi au kutojitambua anaendesha hilo
gari hovyo bila kwa kusahau kuwa kuna alama za barabarani, na matokeo yake huyo
huishia kuparamia nguzo za umeme, au kuparamia makorongo na kuumia vibaya kesho
yake mtu huyo hujikuta akiwa hospital kwa chumba cha watu waliokaribu kukata
roho, huku mikono na miguu yake vimefungiwa bandage n.k hivyo ni kwa msingi huo
hatuwezi kusema kuwa vitu vya namna hiyo na vinginevyo vyaweza tuletea raha
daima katika maisha, ila hivyo huleta raha za muda, raha zenye kupita kuliko
ile raha ya milele.
Leo tunapoadhimisha
jumapili ya nne ya mwaka wa Kanisa tunakumbushwa juu ya raha ya milele jinsi
tunavyoweza kuipata. Mwinjili Matayo katika injili anagusia zile njia za
kuipata raha ya milele, nazo si nyingine bali ni zile heri nane. Daima kama unasafiri pale mahali usipopajua huwa ni
vyema kutembea na ramani ndogo mkononi ili ikupe maelezo halisi ya pale
uendapo. Katika Injili ( Mt 5:1-12) Yesu anatupa ramani ya kutembea nayo ili
hiyo ramani iweze kutufikisha pale raha ya milele ilipo ( ufalma we mbinguni).
Yesu anapoanza utume
wake anaanza kwa kusisitiza kuhusu hizi heri nane, sasa tujiulize kuwa kwa nini
aweke msisitizo katika hizo heri nane? ni kwa sababu ya umuhimu wa hili
fundisho. Kama nilivyoisha elezea hapo awali, ni kwamba kila mmojawetu hapa
duniani huweka juhudi ili mwisho wake apate furaha. Ukifanywa utafiti kwa watu
mbalimbali juu ya nini kiwafanyacho kuwa na furaha yatapatikana majibu
mbalimbali, na yale majibu yakijaribu kulinganishwa na yale majibu Yesu
anayotufundisha katika injili leo, twaweza baini kuwa yatakuwa majibu tofauti.
Pale Yesu asemapo,
" Heri waliomaskini wa roho"
"watu husema heri yao walio matajiri." Pale Yesu asemapo, " heri wenye uzuni"," watu
husema heri yao wale wenye utani." Pale Yesu asemapo, "heri wenye huruma," watu baadala
yake husema, " heri wenye nguvu na hasira." pale Yesu "asemapo heri wenye upole," watu
hesema, " heri yao wale walio maridadi na wenye nguvu." Pale Yesu
asemapo "heri wenye njaa na kiu ya
haki," watu husema, " heri yao wenye mvinyo wa kutosha mezani kwa
ajili ya kusindikiza mlo." Pale Yesu asemapo, " heri wenye moyo safi," watu baadala yake husema, "
heri yao waliobarikiwa kuwa na vitambi na ngozi laini." Pale Yesu asemapo "
heri yao wapatanishi," watu
husema, " heri yao watengeneza habari." Pale Yesu asemapo, " heri yao wadharauliwao na
kushutumiwa" watu baadala yake husema, " heri yao wale ambao wana
mawakili wazuri wa kuwatetea."
Twaweza baini na tambua
kabisa kuwa mafundisho ya Bwana wetu Yesu Kristu juu ya hizo heri nane, ambazo
kimsingi ndoo ramani ituoneshayo njia ya kwenda mbinguni kimsingi zipo kinyume
kabisa na utamaduni wa ulimwengu katika ujumla wake. Kwa kuziishi hizo heri
nane ni kama kupingana na utamaduni ulimwengu. Ni kwamba haiwezekani tukakubali
mafundisho ya Kristu halafu upande mwingine tukakumbatia utamaduni dunia,
tunaalikwa tuchukue kimojawapo na tuache kimojawapo,tuchukue kimojawapo ambacho
ni cha msingi kwetu, ambacho ndoo kinatupeleka katika ile furaha na raha ya
milele.
Tutambue kuwa Yesu katika
mafundisho yake kwetu juu ya hizi heri nane hamaanishi kuwa tuachane na yale
tuyafanyayo, yale yanayotuwezesha kuishi, bali fundisho lake kwetu sote ni
kwamba kwa yale yote tuyafanyayo tumtangulize Mungu mbele kwanza, tutumie yale
yote tuliyonayo kama nyenzo ya kutufikisha kwa Mungu baadala ya kutuangamiza.
Mfano, kama unamiliki simu ya gharama, basi tumia hiyo fursa ya kumiliki simu
ya gharama kuwainjilisha watu, kuwaletea watu habari njema, kurahisha
mawasiliano muhimu, kuliko kuitumia hiyo simu ya ghrama kufanya yasiyopendeza
machoni pa Mungu, kama una utajiri wa pesa, basi tumia hizo pesa kwa kuwasaidia
wale wasiojiweza baadala ya kutumia hizo pesa kwa mambo yasiyo ya lazima na
msingi, kama umejaliwa na akili nyingi, tumia hiyo akili yako nyingi
kuwahelimisha watu, kufanya uvumbuzi kwa ajili ya kuleta maendeleo baadala ya
kutumia hiyo akili kufanya uvumbuzi wenye kuleta maangamizi kwa wengine. Kama
umejaliwa kipaji tumia hicho kipaji kwa ajili ya kumtukuza Mungu baadala ya
kutumia hicho kipaji kujitukuza mbele ya wengine. Kama umejaliwa kupenda nguo,
basi penda nguo ambazo ukizivaa hazileti aibu kwa wengine, nk. Ni kwa msingi
huo ni lazima yale tuliyo nayo tuyatumie katika kuhakikisha kuwa yanatufikisha
mahali ambapo kuna raha ya milele.
Hizo heri nane
tulizozisikia katika Injili siyo kuwa hizo heri zinalenga watu wa aina nane
duniani ambapo tweweza weka maswali na kujiuliza daima kuwa mimi/fulani
anaangukia katika kundi lipi la hizo heri nane, hapana hizi heri nane ni
mwaliko kwa kila mmoja wetu kujitafakari na kubadilika kwa kuelekea kwa Kristu
zaidi. Swali la motisha kwetu ni kwamba maisha yetu huwa yanazamia upande gani
zaidi? katika kumwelekea Kristu au duniani zaidi? Kwa kuishi mafundisho ya
Kristu ni uhakika wa kuipata ile raha ya milele.
No comments:
Post a Comment